Picha: Wachezaji wa England wapiga kambi ndani ya Jeshi lao la Ulinzi - MKWELITZ BLOG

.

demo-image-Recovered

.

Capture

Tuesday, June 6

Picha: Wachezaji wa England wapiga kambi ndani ya Jeshi lao la Ulinzi


96358604_england_mod
Timu ya Taifa ya Uingereza yaweka kambi katika jeshi lao la ulinzi wa majini ili kujiweka fiti kwaajili ya michezo inayo ikabili kikosi hiko cha simba watatu.

Kikosi hiko kinaamini kuwa kufanya mazoezi ndani ya kambi ya jeshi lao tiifu itawaongezea hamasa na uimara ndani ya timu kuelekea mchezo wao wa Jumamosi wa kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Scotland na kisha kukutana na timu ya taifa ya Ufaransa.

Timu ya Taifa ya Uingereza itaikabili timu ya Scotland Jumamosi wa kuwania kucheza Kombe la Dunia

Wadau wa soka nchini Uingereza walishitushwa wakati meneja wa kikosi hiko , Gareth Southgate kuamuru kambi yao ikafanyike katika kambi za mafunzo ya Comando wa jeshi huko Devon.

Wachezaji 22 wa timu ya taifa ya Uingereza ambao walikuwa mapumzikoni baada ya msimu wa ligi kumalizika walikubaliana na mawazo ya kocha wao kwa kambi ya timu hiyo ipelekwe katika kambi za Jeshi.

“Tunahitaji kuwapeleka vijana wetu katika mazingira tofauti ambayo wao hawakuyatarajia,”

“Jeshi lilisema tuwafanyie wachezaji wetu kitu ambacho kisicho tarajiwa na hiyo ilikuwa ni moja ya mtazamo wetu wa kambi”. Gareth Southgate aliliambia shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza FA.

96358606_southgate_mod

96358943_england_mod2

96359663_defoe_mod

96359664_sterling_mod

ENGLAND-FOOTBALL-TEAM-VISIT-CTCRM

96358943_england_mod2

96359664_sterling_mod

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad