Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema Ngoma bado ni mchezaji wa Yanga na amemuaga anakwenda kutibiwa huku Mkwasa akiongeza kwamba bado hawajapokea ofa kutoka klabu yoyote kuhusu kumtaka Ngoma.
“Suala lake lina zungumzika vizuri tu, bado anamajeruhi na ameniomba ruhusa anakwenda kupata matibabu lakini bado tupo naye na anapenda bado awe na sisi lakini ana suala lake kubwa ambalo linamsimu kama unakumbuka muda mrefu hajacheza kutokana na maumivu yanayomkabili.”
“Amekwenda kwa ajili ya ‘deep treatment’ kwa hiyo atakapokuwa amepona tutakuwa nae, kwa mujibu wa mkataba bado ni mchezaji wa Yanga kwa sababu hatujapata ofa kutoka sehemu yoyote na tunachofahamu sisi ni kwamba anaendelea na matibabu kwa hiyo hatuwezi kusema chochote.”
Ngoma hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara huku kukiwa taarifa ambazo si rasmi zikidai kwamba mchezaji huyo anaweza kuihama Yanga na kwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment