Habari zilizonifikia muda huu kutoka Dar es salaam ni kuhusu kifo cha mke mdogo wa Mwimbaji wa zamani wa Jahazi Modern Taarabu Alhaj Mzee Yusuph Chiku amefariki usiku huu wakati anajifungua na mtoto naye amefariki.
Innalillah wainaillah rajuun mke mdogo wa Mzee Yusufu Chiku amefariki dunia usiku huu alipokuwa akijifungua na mtoto amefariki taarifa zaidi tutaendelea kupeana!!
Chiku amekutwa na mauti jana Jumamosi June 17,2017 jioni katika hospitali ya Amana, Ilala ya jijini Dar es Salaam alipopelekwa kujifungua.
Mzee Yussuf amesema alimpeleka mkewe Hospitalini hapo June 17,2017 saa 10 alasiri kwa ajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya alikutwa na mauti hayo baada ya upasuaji uliofanywa kutokwenda salama hivyo kusababisha kumpoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMINA.
No comments:
Post a Comment