Msemaji wa jeshi la wanamaji Ayoub Qassem amesema kuwa polisi hao wamekamata wakimbizi 906 wakiwemo wanawake 92 na watoto 25 katika operesheni iliyofanyika kilomita saba kutoka katika mji wa Sabratha.
Kwa mujibu wa habari,Libya imekuwa ni sehemu muhimu kwa wakimbizi haramu kupita kutoka Afrika kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean ndani ya miaka kadhaa iliyopita.
Bahari ya Mediterranean imepokea takriban wakimbizi 60,521 kufikia leo na asilimia 80 kati yao walifika Italia huku 1530 walifia njiani wakijaribu kuivuka bahari hiyo.
No comments:
Post a Comment