Baraza la Habari lamkaanga RC Makonda - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, August 14

Baraza la Habari lamkaanga RC Makonda


Leo Agosti 14 2017 Baraza la Habari Tanzania chini ya katibu wake mtendaji Kajubi Mkujanga imezunduliwa ripoti ya tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group.

Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwanasheria mwandamizi Juma Thomas ambaye ni Mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na watu wanne, imesema Kitendo cha Makonda kwenda kwenye kituo cha Clouds Media ni kukiuka na kinyume cha Huduma za vyombo vya habari ambapo ripoti hiyo imeweka wazi kuwa Makonda aliingilia uhuru wa Vyombo vya habari na Uhariri wa Habari.
Ripoti hiyo inasema Makonda alitafutwa na timu ya uchunguzi bila mafanikio, na hata walipomwandikia barua hakuna chochote alichojibu, kwahiyo alijiondolea mwenyewe haki ya kusikilizwa.


Hata hivyo ripoti hiyo imependekeza Mkuu huyo wa mkoa kuomba radhi sio tu kwa Wanahabari bali watanzania wote kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here