Mtu mmoja Akamatwa na dawa za kulevya - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, August 14

Mtu mmoja Akamatwa na dawa za kulevya


Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Mohammed R. Mpinga.

Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Faraja Peter kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi kavu kilo 21.6 zikiwa ndani ya nyumba yake pamoja na miche mitatu ya bangi.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Mohammed R. Mpinga wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema mtuhumiwa huyo alikutwa ameficha bangi hiyo kwenye gunia na kuotesha miche hiyo ya bangi kwa kuichanganya na miche ya nyanya nyuma ya nyumba yake katika Kijiji cha Kapwili Kusini, kata ya Kapwili Tarafa ya Unyakyusa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.

Mbali na hilo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Edward White mkazi wa eneo la Matenki Kasumulu akiwa na lita 7 za pombe moshi (gongo) akitokanayo nchi jirani ya Malawi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here