Maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kali kunyesha kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa habari,walioathirika sana ni wale waliokuwa wakiishi maeneo karibu na ziwa Albert.
Maafisa wa serikali walielezea kwamba utafutaji na uokoaji wa watu waliokuwa wamenaswa ulifanyika kwa ugumu sana.
Wengi waliopoteza maisha ni wale waliofunikwa katika maporomoko hayo.
No comments:
Post a Comment