Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Jaqline Nyantori ambapo amedai kuwa kati ya June 28 na July 4, 2017 Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kuwa ni Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu kwa mtu anayeitwa Ladslaus Matindi.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lakini hata hivyo, mshtakiwa alikana kosa lake na upande mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika.
Mshtakiwa huyo alipewa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya Tsh. Milioni Moja na kesi imeahirishwa hadi August 23, 2017.
No comments:
Post a Comment