African Lyon yawawekea pingamizi wachezaji 19 - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 15

African Lyon yawawekea pingamizi wachezaji 19


Dar es Salaam. Timu ya African Lyon imewawekea pingamizi wachezaji wake 19, akiwemo kipa Youth Rostand aliyejiunga na Yanga.

 Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Alfred Lucas alisema Kamati ya Katiba na Hadhi za Wachezaji itakutana kuanzia  Alhamis hii kupitia mapingamizi hayo ili kuweka kila kitu sawa kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza.

"African Lyon imeondokewa na wachezaji wengi waliohamia klabu nyingine na imewawekea pingamizi wachezaji wake 19 wakidai ada za uhamisho kutoka klabu walizotimkia, ada ya maendeleo, na ada ya kuvunja mkataba"

" Pia, Kagera Sugar imemuwekea pingamizi Mbaraka Yusuph kwa madai bado ni mchezaji wao kwani ana mkataba na klabu hiyo, hivyo mapingamizi yote yatapitiwa na Kamati ya katiba na Hadhi za wachezaji ambayo inaweza kukutana kuanzia Alhamis," alisema Lucas.

Alfred aliwataja wachezaji hao wa African Lyon ambao wamewekewa pingamizi kuwa ni Rostand(Yanga), Saleh Malande (Majimaji), Hamad Manzi, Mussa Nampaka, Lambele Jerome(Lipuli), Hamad Waziri, Baraka Majogoo(Ndanda), Omary Salum, Fred Lewis (Coastal Union), Abdallah Mguhi, Omary Abdallah, Venance Ludovic (Kagera Sugar).

Pia, alisema Azam imewekewa mapingamizi mawili dhidi ya Kagera Sugar wanaopinga kusajiliwa kwa mshambuliaji wao Mbaraka Yusuph na dhidi ya Majimaji wanaopinga kusajiliwa kwa mchezaji wao Iddi Kipangulile.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here