Msemaji wa waziri wa ulinzi Ahmed Arab amesema kuwa askari aliyepoteza maisha ni kati ya askari majasiri na alikuwa akijaribu kuzuia shambulizi hilo kutokea.
Kwa mujibu wa habari,aliyekuwa amelengwa hasa katika shambulizi hilo ni Jenerali Hussein Hassan Osman,ambae ni kamanda wa vikosi vya ulinzi.
Ripoti zinaonyesha kuwa kamanda aliyekuwa ndani ya jela hiyo wakati wa shambulizi amenusurika.
Kundi la kigaidi la Al Shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Mpaka sasa haijajulikana bado ni vipi mtu aliyejilipua aliweza kupita ukaguzi wa usalama mpaka kuingia ndani ya jela hiyo.
No comments:
Post a Comment