Niyonzima awatoa hofu Simba - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, August 19

Niyonzima awatoa hofu Simba


Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda.

KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, ametuliza mzuka wa mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa, wasiwe na wasiwasi juu ya matokeo yasiyoridhisha wanayoyapata katika baadhi ya mechi zao za kirafiki.

Juzi Alhamisi usiku, Simba ilitoka suluhu na Mlandege FC kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema hata wao matokeo hayo hawayafurahii, lakini wanaendelea kupambana kuhakikisha kabla ya msimu wa ligi haujaanza, wawe na kikosi imara kitakachokuwa kinawapa matokeo mazuri kila siku.

“Unajua katika soka kuna kushinda, sare na kufungwa, lakini hakuna timu inayopenda kufungwa, ndiyo maana Mlandege nao walikuwa wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi kama sisi hali iliyofanya mchezo kumalizika kwa suluhu.

“Lakini mashabiki wanatakiwa kutulia na kuendelea kutupa sapoti kwani kikosi kinaandaliwa kwa ajili ya kufanya vizuri katika ligi, hivyo imani yangu ni kwamba tutakuwa hatari ligi ikianza, mashabiki watulie tu,” alisema Niyonzima.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here