Tshishimbi awa gumzo zaidi ngao ya Jamii - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, August 24

Tshishimbi awa gumzo zaidi ngao ya Jamii


Kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi ndiye gumzo zaidi katika wachezaji waliocheza mechi ya Ngao ya Jamii baina ya watani wa jadi, Yanga na Simba.

Simba na Yanga zilikutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana na mwisho, Simba wakaibuka na ushindi wa mikwaju 5-4.

Tshishimbi raia wa DR Congo ambaye amejiunga na Yanga akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland ndiye amekuwa kipozeo cha machungu ya mashabiki wa Yanga baada ya kupoteza mchezo huo. Kwani ilikuwa ni mechi yake ya kwanza lakini akafanikiwa kuonyesha kiwango cha juu zaidi.

Tshishimbi alionyesha kiwango cha juu katika mechi hiyo huku akikaba kwa kunyang’anya mpira na baadaye kusaidia kuichezesha.

Kiungo huyo Mkongo alishirikiana kwa kiwango cha juu na uelewano mzuri na kiungo mwingine wa Yanga, Thabani Kamusoko ambaye naye alionyesha kiwango kizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here