Mahakama ya mjini Middleburg mji ulioko kilomita 160 kutoka jiji la Pretoria imewatia hatiani wakulima wawili weupe baada ya mkanda wa video kutapakaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mkanda huo ulionyesha jinsi wakulima hao weupe walivyokuwa wanamwingiza kwa nguvu mtu huyo mweusi ndani ya jeneza na kutishia kuliwasha moto jeneza hilo.
Tukio hilo limesababisha mgawanyiko wa hisia katika nchi ambayo inakabiliwa na ubaguzi wa rangi hata baada ya kumalizika kwa utawala wa kibaguzi miaka 23 iliyopita.
Mtu huyo mweusi ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba amefurahishwa na hukumu hiyo kwani hatimae haki imetendeka.



No comments:
Post a Comment