Wolper amtolea povu la nguvu Madee - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 15

Wolper amtolea povu la nguvu Madee



DIVA anayeng’ara kupitia Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, amejikuta akimtolea povu staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ kwa kosa la kutumia katuni ya picha yake bila ridhaa yake kwenye kideo cha ngoma yake ya Sikila aliyomshirikisha staa wa muziki nchini Nigeria, Tekno.

‘Jini Mkatakamba’ wa Wolper alipanda baada ya kuona video hiyo na ndani ya dakika sifuri akawahi kwenye mahakama kuu ya watu maarufu yaani Instagram na kuposti  picha ya katuni yake inayopatikana kwenye video hiyo kisha kuiambatanisha na ujumbe ufuatao:

“Hebu ona jamani, macho yanatia huruma kama nina upwiro kilo 200. Hii mikaka yetu ya Kibongo kuna muda inaboa, kuna muda inakuwa poa. Sasa Madee, Rais wa Manzese nikuulize swali, ulishindwa nini kunyanyua ka simu kako na kunipigia hata kinafiki na kuniambia unani-video queen katuni, sijui sanamu?

“Unajua wewe, acha dharau, wewe pumbavu, piga simu, omba kwanza, hata kama humlipi mtu, sisi tunasaidiana, wote wasanii, leo kwangu, kesho kwako
na kunishika kimahaba, umenishika, una dhambi wewe kaka na suti umenivalia kama unaenda kutoa posa kwa Masawe.

“Sasa onyo, siku nyingine omba utapewa, acha kuparamia kama vile unaomba raundi kwa kimada wako, kwanza unitafute utoe hata faini ya kuniweka macho kama nimevuta ugoro.

“Ila nyimbo kali, nisiwe mchoyo na nimependa idea ila mwambie alinichonga na kunipa hiyo shepu nitampasua.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here