Ibra Kadabra katika msimu uliopita wa ligi aliifungia Manchester United mabao 28 katika michezo 46 aliyoichezea United lakini majeraha yalimfanya kutomaliza msimu uliopita.
Taarifa kutoka Manchestet United imethibitisha kwamba klabu hiyo imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mchezaji huyo na sasa anakwenda kuvaa jezi namba 10.
Kadabra amesema “nina hamu sana kurudi tena Old Trafford lakini najua ninapaswa kupambana ili kuwa tayari, nimekuwa nikifanya sana mazoezi na nitaendelea kujituma niwe tayari kwa msimu”
Kwa uwezo na upambanaji wa Ibrahimovich na uwepo wa Romelu Lukaku katika kikosi cha United inaweza kuwa pacha mpya hatari zaidi katika ligi kuu nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment