Tanzia: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni (2012) afariki dunia - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, September 3

Tanzia: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni (2012) afariki dunia


Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni (2012) na nguli wa habari nchini, Rweyemamu Muhingo(67) amefariki leo  katika hospitali ya Aga Khan jijini.

Muhingo ameacha  simanzi katika tasnia ya habari, familia na taifa kwa ujumla.

Muhingo ambaye awali alibahatika kuteuliwa na Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuongoza wakazi wa Halmashauri ya Handeni kabla ya kuhamishiwa Makete na baadaye Morogoro mjini.

Kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi linalochapisha magazeti ya Mwanaspoti na The Citizen. Pia aliwahi kuandikia gazeti la Mtanzania

Mtoto wa marehemu, Mwesigwa Muhingo ameliambia gazeti hili leo kwamba, amefariki kwa maradhi ya Myelofibrosis, yanayotokana na mifupa kushindwa kutengeneza damu.

 “Alhamisi tulikuwa na mpango wa kumsafirisha nje ya nchi ingawa tulikuwa hatujapata  hospitali  hali yake ilibadilika  ghafla leo saa 3:00 Mungu akamchukua’’amesema Muhingo.

Mwananchi:

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here