Uhuru, Odinga walivuruga baaza la mitihani Kenya - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, September 3

Uhuru, Odinga walivuruga baaza la mitihani Kenya


Uchaguzi mpya wa Urais unaotarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kuanzia Septemba 30 nchini Kenya, unatajwa kuvuruga ratiba ya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari inayotarajiwa kuanza sambamba na uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini Kenya kwenye Baraza la mitihani nchini humo, mitihani hiyo inatarajiwa kuanza Oktoba 31 na Novemba 6, huku uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Novemba 1 mwaka huu.

Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi ambayo itafanyika ndani ya siku 3 inatarajiwa kuisha Novemba 2 wakati ile ya sekondari inatakiwa kufanyika ndani ya wiki 3.

Katibu wa Baraza la Elimu nchini humo Fred Matiang’i anakusudia kukutana na Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC ili kutafuta njia mbadala ya kukabilianaa na hilo, ikiwezekana uchaguzi ufanyike tarehe nyingine, ikizingatiwa kwamba vyumba vya madarasa ya shule nyingi za umma hutumika kama vituo vya kupigia kura.


Uchaguzi mpya wa Urais unatarajiwa kufanyika baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi wa Uhuru Kenyatta kufuatia uchuzi wa Agosti 8, baada ya kumaliza kusikiliza kesi ya uchaguzi wa Urais iliyofunguliwa na Muunganiko wa vyama vya upinzani nhini Kenya, NASA.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here