Tuzo za Pan African 2017 kufanyika Tanzania - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 16

Tuzo za Pan African 2017 kufanyika Tanzania

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za panafrican almaarufu kama Pan African humanitarin awards pamoja na mkutano mkubwa wa masuala ya kidiplomasia amani na na misaada ya kibinadamu katika bara la Afrika zitakazo fayika siku ya juma mosi katika ukumbi wa LAPF Kisenga international conference centre Jini dar es salaam.

akiongea na waandishi wa habari mratibu mkuu wa Tanzania katika kamati ya maandalizi ya Tuzo hizo Suleima Kitenge amesema kuwa wao kama asasi ya vijana wa umoja wa mataifa ndio wanaondaa tuzo hizo
" Naomba nieke msistizo kuwa yuna kama asasi wanasmama kama waandaaji tu amabo watakuwa wanahusika kama waandaji wa mkutano tu" Aidha Kitenge aliongeza kuwa tuzo hizo hazihusishi upigaji kura bali kuna kamati maalumu ya inayofanya utafiti na kuchagua wawaniaji tuzo kamati inayoongozwa na Brigedia Walles Williams.

kitenge amesema kuwa tuzo hizo zilianza kufanyika nchini Ghana mwaka 2015 huku Hubai zikifanyika mwaka 2016 na kusema kuwa sasa ni fursa kwa nchi ya Tanzania kwani tuzo hizo zinazoandamana na mkutano wa kidiplomasia zitaeiletea nchi manufaa mengi." Kwakua kutakua na wageni wengi maarufu na wenye nyadhfa kubwa itapelekea nchi yetu kunufaika na mambo mengi"

kwa upande wake mmoja wa wadhamini wa maandalizi hayo kutoka katika kampuni ya mtandao ya RAHA LTD Bi Mahbib Jemedari amabaye ni meneja masoko amesema kuwa kamapuni yao itashirikiana nao katika kila hatua mpaka watakapo fanikisha maandalizi hayo."kampuni ya Yona imekuwa ikitoa huduma Tanzania kwa takriban miaka 20 sasa na tutashirikiana na Asasi ya vijana wa umoja wa mataifa mpaka wakamilishe maandalizi"

Naye mtaalamu wa mawasiliano katika asasi hiyo bwana Paul Siniga amesema kuwa shughuli hiyo itapambwa na mabalozi wa umoja huo kutoka hapa nchini"kuna mabalozi amabao wanawakilisha vijana wapo hapa nchini na niwatu maarufu pia watakuwepo"

Itakumbukwa kuwa Tuzo hizo hazijawahi kupata mshindi kutoka Tanzania katika tuzo hizo amabazo huwahusisha watu kutoka nchi mbalimbali wakliofanya vizuri katika huduma za kijamii.

mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibara Doka Ali Mohamme Shein


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here