Bastian kwenye kikosi Man United - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, September 2

Bastian kwenye kikosi Man United

Na Annel James

KIUNGO Mjeruman wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa klabu hiyo kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu.













 Katika siku za karibuni kulikuwa na taarifa kuwa meneja wa United Jose Mourinho alikuwa amemuhabalisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 kuwa anaweza asiichezee tena.

 Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani amestaafu soka lake la kimataifa mapema wiki hii baada ya kufunga mabao 24 katika mechi 121 alizoichezea. Klabu zote 20 za Ligi Kuu zilipaswa kuwasilisha majina ya wachezaji 25 watakaowatumia katika Ligi Kuu, jana.

 Schweinsteiger ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu Julai mwaka jana, amekuwa akifanya mazoezi peke yake na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23 toka Mourinho akabidhiwe mikoba kiangazi hiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here