Shule nne Wilayani Geita zanufaika na Madawati Tigo Fiesta - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 1

Shule nne Wilayani Geita zanufaika na Madawati Tigo Fiesta

Na Mustafa Ismail

Kampuni ya mtandao ya  Tigo leo imekabidhi madawati 185 yenye thamani ya shilingi milioni 31  yatakayogawiwa  kwa shule nne katika mkoa wa Geita  ikiwa ni sehemu ya mkakati wake unaoendelea nchi nzima wa kutoa msaada wa madawati  ambayo yatainufaisha mikoa mine kwenye tamasha la fiesta 2016














Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo  zilizofanyika katika Shule ya Msingi Mwatulole, Meneja wa Kikanda wa Tigo Kanda ya Ziwa Edgar Mapande, alisema kuwa  umekuwepo uhitaji mkubwa wa madawati katika shule za msingi na kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawati  imebainika kuwa ni moja ya sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza  pamoja na ufanisi wa masomo miongoni mwa  wanafunzi  katika  shule zetu nyingi za msingi.
“Lengo letu kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi na tunayo furaha  kwamba msimu wa FIESTA 2016 unaleta mabadiliko kwa  kizazi cha baadaye  ambacho ni wanafunzi walio katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai tena chini sakafuni,” alisema Mapande.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu  Ezekiel Kyingu     ambaye alisema kuwa madawati hayo 185 yataboresha kwa kiwango kikubwa  mazingira ya kujifunza  kwa watoto katika mkoa huo  na kutoa witom kwa watu wengine wenye mapenzi mema  kujitokeza  na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mashule  mkoani humo.
Kyingu  alizitaja shule  zitakazonufaika na  madawati hayo  na idadi yake katika mabano kuwa ni Mwatulole (50), Nyankumbu (45), Ukombozi (45),  na Kivukoni (45).
 “Tunawashukuru sana Tigo  kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza idadi ya uhaba wa madawati  katika shule za msingi mkoani Geita. Tunaamini  madawati haya 185  yatatufikisha mbali  katika  kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika kuelekea kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Kyingu.
Hadi sasa tigo ishatoa msaada wa madawati kwa mkoa wa kagera na Kahama

jukumu la kusukuma gurumu la elimu nijukumu la kila mtanzania hivyo basi tushirikiane katika kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu bora na sio bora elimu kwa kuchangia madawati kwa namna moja au nyengine





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here