Umoja wa Mataifa UN umeihimiza kuwepo kwa utulivu nchini Gabon baada ya fujo kuzuka kuhusiana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.
Baraza la
Usalama la umoja huo limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake kujizuia
kufanya uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za kisheria.
Maafisa wa
usalama kufikia sasa wamewakamata watu zaidi ya elfu moja baada ya siku ya pili
ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.
Upinzani
unadai Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi
Watu watatu
waliuawa mji mkuu Libreville.
Rais Bongo
amesisitiza kwamba alishinda kwa njia halali na kuutaja ushindi wake kuwa
ushindi wa watu wa Gabon.
Matokeo ya
uchaguzi yalitangazwa Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi kwa 49.8%
ya kura, akifuatwa na Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura zilizowatenganisha
zikiwa 5,594.
Bw Ping
alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na "hakuna ajuaye" hasa nani
alishinda.
Upande wa Bw Ping unasema takwimu kutoka ngome za rais huyo zinaonyesha
asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza. Ameomba takwimu za wapiga kura kutoka
kila kituo zitolewe wazi.
Bw Bongo
aliingia madarakani mwaka wa 2009, baada ya kifo cha babake aliyekuwa ameongoza
taifa hilo tangu 1967.
Kabla ya
kuingia katika siasa, Ping aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa
Afrika.
No comments:
Post a Comment