Nahodha wa
Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameiangalia timu hiyo kwa umakini na kisha
kutoa onyo kwa wachezaji wenzake kutokana na hali inayoendelea kwa sasa ndani
ya kikosi hicho.
Cannavaro
ameanza kwa kueleza kuwa, Ligi Kuu Bara msimu huu iliyoanza wiki mbili
zilizopita ipo tofauti na ushindani wa ligi za misimu ya nyuma.
Beki huyo
anamaanisha kuwa, ligi ya sasa ushindani umeongezeka zaidi na kama wachezaji
wenzake wataendeleza masihara, basi wanaweza wasifanye lolote msimu huu.
Cannavaro
alisema licha ya ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya African
Lyon, bado wanahitaji kubadilika kama kweli wanahitaji mafanikio msimu huu.
“Nimefurahi
tumeshinda mechi ya kwanza na Lyon lakini ukiangalia tulibebwa na ugeni wa Lyon
kwenye ligi na ile ‘experience’ ya mechi nyingi za kimataifa tulizocheza lakini
kama Lyon ingekuwa makini siku ile, tungepata shida sana.
“Kuhusu
kikosi, wala hakina tatizo, tumekamilika vizuri tu, lakini tatizo ni masihara
na kujiamini kwingi, mechi ya Ngao ya Jamii tuliyocheza na Azam hatukupaswa
kuipoteza.
“Lakini
kimasihara tukafungwa, sasa kama tutaendelea hivi, sidhani kama tutafanikiwa
msimu huu na ukitazama ligi ya sasa ni ngumu."
No comments:
Post a Comment