Wasiosoma elimu ya juu walalama kudaiwa mikopo - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, September 3

Wasiosoma elimu ya juu walalama kudaiwa mikopo

 Na Mustafa Ismail

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya majina ya wadaiwa sugu wa mikopo hiyo,jambo lililoibua taharuki kwa baadhi ya watumishi wilayani Namtumbo, Ruvuma baada ya kuingizwa kwenye orodha hiyo huku baadhi yao wakidai hawajasoma elimu ya juu au kuhusika na kuomba mkopo huo.
Ofisa Habari wa Wilaya ya Namtumbo, Yeremias Ngerangera alithibitisha kupokea malalamiko ya walimu sita wa shule za msingi ambao wanadai hawajasoma elimu ya juu wala kuomba fedha hizo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Ngerangera aliwataja walimu waliowasilisha malalamiko kuwa ni Thomas Komba anayedaiwa Sh milioni 3.4, Joseph Chengula anayedaiwa Sh milioni 12.9 na Michael Haule anayedaiwa Sh milioni 2.7.
Aliwataja wengine kuwa ni Michael Jimmy anayedaiwa Sh milioni 29.1, Deogratias Haule anayedaiwa Sh milioni 16.0 na Marry Haule anayedaiwa Sh milioni 2.6 ambao wanailalamikia bodi kuwadai fedha hizo wakati hawajakopa wala kusoma kwa fedha za bodi hiyo.

Hata hivyo, Ngerangera alisema Halmashauri ya Wilaya Namtumbo inaendelea kupokea malalamiko hayo ya walimu kwa maandishi ili kuwasilisha Bodi ya Mikopo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kubaini ukweli wa madai hayo.


Hadi kufikia sasa Mwalimu Komba na Chengula ndio waliofika katika ofisi ya Ofisa Habari ili kujua ukweli zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here