Mwanzilishi
wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amelezea kusikitishwa kwake baada ya
satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya kasi ya mtandao wa
intaneti barani Afrika kuharibiwa.
Satelaiti
hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la
Florida, Marekani siku ya Alhamisi.
Satelaiti
hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo
ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya
Jumamosi.
Mlipuko huo
ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo
yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.
Bw
Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, amesema "nimesikitishwa sana"
kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa.
"Tutaendelea
kujitolea katika lengo lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na
tutatia bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na
satelaiti hii," aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hakuna
aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo.
Afisa mmoja
wa masuala ya anga za juu wa Israeli amesema satelaiti ya Amos-6 inakadiriwa
kuwa na thamani ya $200m (£150m) na ilimilikiwa na kampuni kwa jina Spacecom,
was a major blow to the industry.
"Hili
ni pigo kubwa sana ambalo huenda ikaathiri mustakabali wa sekta ya satelaiti na
huenda ikahitaji kupigwa jeki (kifedha)," alisema mwenyekiti wa taasisi ya
masuala ya anga za juu ya Israel, Isaac Ben-Israel.
No comments:
Post a Comment