CLATTENBURG KUAMUA MCHEZO WA DARBY YA MANCHESTERMARK - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, September 6

CLATTENBURG KUAMUA MCHEZO WA DARBY YA MANCHESTERMARK

Na Anael James Waziri_Tall

Clattenburg ametangazwa kuwa mwamuzi wa mchezo wa mwishoni wa wiki hii ambao utawakutanisha mahasimu wa jiji la Manchester.

Mchezo huo utazikutanisha Manchester City inayoongozwa na Pep Guardiola na Manchester United ya Jose Mourinho huku timu zote zikiingia katika mchezo huo zikiwa hazipoteza mchezo toka kuanza kwa msimu huu.

Mike Dean ameteuliwa kuwa mwamuzi wa ziada huku Jake Collins na Steve Bennett wakitarajiwa kushika vibendera kumsaidia Clattenburg.

Clattenburg ndio mwamuzi aliyechezesha fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2015-2016 na ile ya Ulaya iliyochezwa mapema kiangazi hiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here