Na Ebdo Classic
Msanii Fid Q
ambaye ni rapa wa hapa Bongo kutoka pande za Rock City/Mwanza, ametoa sababu
iliyomfanya akavaa koti lililochanika kwenye video yake mpya, na kuleta
minong'ono kwa mashabiki.
Fid Q
amesema aliamua kuvaa hivyo ili kuweza ku'relate na maisha halisi ya mashabiki,
ambao asilimia kubwa wanashindwa kuhimili vitu vya gharama ambavyo wasanii
wanavaa kwenye video zao, na kuhisi kutengwa.
“Unajua ni
muda mrefu wanamuziki wamekuwa wakifanya video, wanavaa vitu ambavyo asilimia
90 ya mashabiki wao hawawezi kuvi'aford', wanakuwa wanavitamani tu, lakini njia
rahisi siku hizi ya kuweza kufikisha muziki ni kuhakikisha kwamba unafanya kitu
ambacho wanaweza waka'relate' nacho, wanaweza wakajihusisha nacho au kikawa
kinawahusu”, alisema Fid Q.
Pia Fid Q
aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kuamua kujihusisha na maisha halisi ambayo
mtaa anaoishi yapo, aliamua kufanya hivyo kama moja ya mtindo wa nguo zake
alizovumbua, akifananisha na ile mitindo ya msanii wa Marekani Kanye West.
“Hatupaswi sana kuwa tunajifanya ndo wasanii
tunavaa vitu vya gharama zaidi, wakati tunawakilisha maisha halisi ya mitaa
ambayo tunatokea, mitaa ninayotokea mimi kuna watu wanavaa majacket ambayo
yameshavaliwa, yamechanika kwa sababu ya shida, kwa hiyo nawakilisha
ninakotokea mimi, kwa hiyo ule ndio uhalisia na ndio fasheni ambayo
nimeivumbua, kama ambavyo Kanye West amevumbua nguozake”, alisema Fid.
No comments:
Post a Comment