FIFA YAWAKUBALIA SUNDERLAND KUSAJILI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 8

FIFA YAWAKUBALIA SUNDERLAND KUSAJILI

Sunderland imemsaini Kipa kutoka Klabu ya Ureno Boavista aitwae Mika kwa Mkataba wa Miaka Miwili bila Ada yake kutajwa.

Kipa huyo Raia wa Ureno mwenye miaka 25 anaweza kuichezea Sunderland Jumatatu ijayo ikicheza na Everton kwenye Ligi Kuu England, EPL, huko Stadium of Light.

Uhamisho huu umefanyika nje ya Dirisha la Uhamisho na kukubalika baada ya FIFA kuridhia kuwa Uhamisho wa Mika ulikwama kukamilika kwa sababu za Kiufundi kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa rasmi Saa 7 Usiku Agosti 31.

Sunderland walilazimika kusaini Kipya mpya kwa dharura baada ya Kipa wao, Vito Mannone, mwenye Miaka 28, kuumia Kiwiko cha Mkono na sasa kulazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here