RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewasihi wananchi wa Pemba na vitongoji vyake wasibabaishwe na wanasiasa wanaowadanganya watu na kusema kuwa Uchaguzi Mkuu umekwisha na hautafanyika mwingine hadi mwaka 2020 na Ali Mohamed Shein ndiye Rais halali wa Zanzibar
Amewakemea
wanasiasa wanaopita kila kona na wakitembea Ulaya, akisema safari zao hizo
zitaishia vichochoroni kwani Rais aliyepo madarakani kwa sasa ni Dk Shein.
“Nataka
niwaambie hao wanaokwenda nje na kujitangaza kwa kujitapa, kwamba Rais aliyepo
madarakani kwa sasa ni Dk Shein......uchaguzi umekwisha na utafanyika mwingine
ifikapo mwaka 2020,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa kwa nguvu na
umati mkubwa wa wananchi.
Rais
Magufuli alisema hayo wakati akihutubia umati wa wananchi wa mikoa miwili ya
kisiwa cha Pemba, ya Kaskazini Pemba na Kusini Pemba katika mkutano wa hadhara
kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale mjini hapa, uliokuwa na lengo la kutoa
shukrani kwa wananchi wa Pemba kwa
kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Alisema
anakerwa na matukio ya vitendo vya chuki na uhasama ikiwemo watu kuchomeana
mali zao ikiwemo mikarafuu, neema ambayo wananchi wamepewa na Mungu.
Alisema
matukio hayo yanafanywa kwa lengo la kujenga chuki na uhasama huku baadhi ya
watu wakiathirika vibaya baada ya kuharibiwa mazao yao.
Aliongeza
kuwa kwamba, wakati akila kiapo cha utii na uaminifu aliahidi kulinda Muungano
pamoja na amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuwaonya
viongozi wanaopandikiza chuki na uhasama kwamba atapambana nao kwa nguvu zote
kwani hakuna uwekezaji katika nchi iliyojaa vurugu.
Aliviagiza
vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinawasaka watu wote wanaofanya vurugu kiasi
kuhatarisha amani na utulivu.
“Mimi
nawashangaa sana watu wa Pemba sijui mnataka nini tena.....mnaye Rais mpole
sana ambaye anatoka Pemba sasa sijui mnataka nini jamani,” alihoji Rais
Magufuli.
Aliwataka
wananchi wa Pemba kutoa ushirikiano wa dhati kwa Rais Shein na kuacha
kuwasikiliza wanasiasa waliofilisika ambao kila siku kazi yao kuwadanganya
wananchi huku wengine wakijidai wanatoka Ulaya kumbe wapo jijini Dar es Salaam
wamejifungia.
“Mimi
namfahamu sana Rais Shein....nilifanya kazi naye mimi tangu nikiwa naibu waziri
wa uvuvi.....huyu uwezo wake ni mkubwa na itumieni hazina yake,” alisema.
Aliwataka
wananchi wa Zanzibar kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kuleta maendeleo
ikiwemo ujenzi wa viwanda mbalimbali ambavyo vitasaidia kuzalisha ajira.
Kwa mfano,
alisema kisiwa cha Pemba kina utajiri mkubwa wa sekta ya uvuvi ambayo ikitumika
vyema itasaidia kuimarisha ajira kwa vijana.
Alisema
amedhamiria kushirikiana na Rais Shein katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya
CCM katika sekta mbalimbali zikiwemo ujenzi wa viwanda pamoja na utalii.
“Nawaombeni
wananchi wa Pemba tufanye kazi pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
katika kuleta maendeleo....hakuna uchaguzi utakaorudiwa jamani,” alisema Dk
Magufuli ambaye ni mara yake ya kwanza kuhutubia hapa, tangu ashinde urais
mwaka jana.
Aidha, Rais
Magufuli aliipongeza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kusimamia uchaguzi
vizuri ule wa kwanza wa Oktoba 25, mwaka jana wa marudio Machi mwaka huu, huku
akimmwagia sifa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha.
“Kama kuna
mtu anayestahiki kupewa tuzo ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,
Jecha Salim Jecha.....huyu mtu ukipata nafasi ya kutoa tuzo basi umuangalie
vizuri sana,”
Dk Magufuli
alisema akimueleza Rais Shein. Tangu kumalizika kwa marudio ya Uchaguzi Mkuu
Machi mwaka huu, viongozi wa vyama vya upinzani hasa Chama cha Wananchi (CUF)
waliosusia uchaguzi huo ambao Dk Shein alishinda kwa kishindo kwa asilimia 91.4,
wamekuwa wakipita ndani na nje ya nchi wakidai uchaguzi huo haukuwa halali.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ndiye
anayesafiri nje ya nchi akieleza kwenda ‘kuishitaki’ Serikali ya Dk Shein
kutokana na malalamiko yao kuhusu uchaguzi huo.
Hali ya Zanzibar
kisiasa bado haijatulia huku wanasiasa wakizidi kushindana kila uchao
No comments:
Post a Comment