Mapacha walioungana wajiandaa kuanza shule London - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 1

Mapacha walioungana wajiandaa kuanza shule London

Na Salum Aboud

Rosie na Ruby Formosa walikuwa wameungana kwenye sehemu yao ya tumbo na walitumia sehemu moja ya utumbo waliyotumia kabla ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa kuwatenganisha mnamo mwaka 2012.











Mama yao , Angela Formosa, amesema watoto hao ambao kwa sasa wana umri wa miaka minne , kutoka eneo la la Bexleyheath Kusini mashariki mwa mji wa London ,"wanafuraha sana " ya kuanza shule.

Miaka mmine iliyopita akilini mwangu sikufikiria kitu kama hiki kingelitokea ," alisema.
"Nilipokuwa mjamzito sikudhani nitaiona siku ya ya kwanza shuleni kwa hivyo inanifurahisha sana kwa hiyo nashukuru sana hospitari ya I Gosh [Great Ormond Street Hospital] kwa kweli.
Nilipokuwa mjamzito sikudhani nitaiona siku ya ya kwanza shuleni kwa hivyo inanifurahisha sana kwa hiyo nashukuru sana hospitari ya I Gosh [Great Ormond Street Hospital] kwa kweli."
Bi Formosa alisema ilikuwa ni taarifa ya ''kuvunja moyo'' kwake na kwa mumewe Daniel Formosa walipogundua kuwa watoto wao wa kike walikuwa na hali ya nadra ya kimatibabu, ambayo hutokea mara moja kati ya watoto 200,000 hai wanaozaliwa .

Watoto hawa wa kike walizaliwa katika hospitali ya Uversity College of London kwa upasuaji mwaka 2012 wakati mama yao Bi Formosa akiwa na ujauzito wa wiki 34.
Baada ya saa kadhaa baada ya kuzaliwa walipelekwa katika hospitali ya Great Ormond Street Hospital kwa ajili ya upasuaji wa dharura kutokana na kuziba kwa utumbo.

Bi Formosa, mwenye umri wa miaka 35, anasema alihisi ni kama " miaka milioni "iliyopita kuwasubiri watoto hao kutoka kwenye chumba cha upasuaji .
" Muda umekwenda, siwezi kuamini jinsi muda ulivyokwenda haraka ," alisema.
" Wanafanana sana, wanaakili sana na bidii , ambayonaifahamu walikua nayo ndani ya tumbo yangu kwa sababu waliendelea kukua na kujitahidi kuishi
Profesa Paolo De Coppi, mtaalamu wa upasuaji wa watoto katika hospitali ya Gosh, amesema : "Tunafurahi kwamba Rosie na Ruby wanaanza shule Septemba mwaka huu.

Visa vya watoto kuzaliwa wakiwa wamegandana hutokea mara kwa mara katika nchi tofauti huku madaktari na wanasayansi wakifanya juhudi zote kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto hao

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here