NAHODHA WA ENGLAND WAYNE ROONEY KUWEKA REKODI LEO. - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, September 4

NAHODHA WA ENGLAND WAYNE ROONEY KUWEKA REKODI LEO.

Na Anael James


Leo usiku Wayne Rooney anaenda kuweka rekodi mpya pale England itakapovaana na Slovakia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 utakaochezwa majira ya 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Rooney anaenda kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kuwahi kutokea katika Timu ya Taifa ya England kwa kucheza michezo 116.
Kabla ya mchezo huu wa leo, Rooney anafungana na David Beckham wote wakiwa wamecheza michezo 115.

Zaidi ya hapo, Rooney pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwenye taifa hilo kwa kufunga mabao 53.
Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Allan Shearer alinukuliwa akisema ni wakati wa Rooney sasa kujiengua England na kuwaachia vijana, hali iliyopingwa vikali na Rio Ferdinand ambaye alisisitiza Rooney aendelee kubaki ili kutoa uzoefu zaidi kwa Vijana.

Hivyo kuelekea mchezo huo, David Beckham amemimina pongezi kwa nahodha huyo wa England kwa mafanikio hayo makubwa anayoenda kuyapata.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here