RONALDINHO KUSTAAFU SOKA RASMI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 8

RONALDINHO KUSTAAFU SOKA RASMI

Na Anael James Waziri_Tall

NYOTA wa zamani wa kimataifa wa Brazil na klabu za Barcelona na AC Milan, Ronaldinho amebainisha nia yake ya kutaka kutundika daruga zake baada ya kupita miaka 18 akisakata kabumbu barani Ulaya na Amerika Kusini. 

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36, ni mmoja kati ya wachezaji wachache kuwahi kunyakuwa mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na lile la Copa Libertadores na pia amewahi kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Brazil mwaka 2002. 

Lakini kushindwa kwake kutulia katika klabu moja toka alipoondoka Atletico Mineiro mwaka 2014 kunamfanya kufikiri kuwa wakati wake wa kustaafu umefika. 

Akizungumza na wanahabri jijini New York, Ronaldinho amesema kwasasa ameshakuwa mtu mzima na sio Ronaldinho yule aliyekuwa na miaka 26 waliyemzoea. Nyota huyo alindelea kudai kuwa anadhani wakati wake wa kustaafu umefika na atafanya hivyo baada ya kucheza kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here