XHAKA APATA SHAVU KWA KOCHA WA USWIZI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 8

XHAKA APATA SHAVU KWA KOCHA WA USWIZI

Na Anael James Waziri_Tall

Kocha wa Uswizi Vladimir Petkoviv amemuunga mkono kiungo wa ARSENAL Granit Xhaka baada ya kutolewa  nje katika mchezo walioshinda goli 2-0 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya Ureno jana Usiku.

Xhaka mwenye umri wa miaka 23 alitolewa nje ya uwanja katika dakika ya 90 baada ya kuzawadiwa kadi ya pili ya manjano katika mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2018.

Nyota huyo sasa anatarajia kukaa nje katika mchezo ujao dhidi ya Hungury Oktoba 7,lakini anaweza kurejea katika mchezo dhidi ya Andorra siku tatu baadae.

Akihojiwa Petkovic amesema kuwa kadi hizo mbili zilikuwa nyepesi hivyo hakustahili kupewa kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here