Wafanya biashara waandamana Nairobi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, September 2

Wafanya biashara waandamana Nairobi

Na Mustafa Ismail

Mamia ya wachuuzi waliokasirika wamefanya maandamano katika barabara za eneo la Eastleigh jijini Nairobi ili kupinga kuvunjwa kwa vibanda vyao.











Usiku kucha maafisa wa polisi waliharibu vibanda vilivyojaa kandokando ya barabara ambapo huweka bidhaa zao zote.

Operesheni hiyo ya polisi inafuatia malalamishi kutoka kwa wamiliki wa maduka ambao wanasema kuwa wamekuwa wakizuia watu kuingia katika maduka hayo.

Wamiliki wa maduka pia nao wamefunga maduka yao ikiwa ni mgomo wao wa siku tatu wa kutaka baraza la jiji la Nairobi kuwandoa wachuuzi hao.

Visa kama hivi vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika mji wa Nairobi huku serikali ikitupiwa kidole cha lawama.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here