MUANGALIE HAPA MWANAMKE ANAYEJIITA "MUNGU" ALIYEUWA WATU NCHINI INDIA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, November 19

MUANGALIE HAPA MWANAMKE ANAYEJIITA "MUNGU" ALIYEUWA WATU NCHINI INDIA

Polisi nchini India wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliye mafichoni baabda ya kufyatua risasi za kusherehekea kwenye harusi
Hakuna mengi kumhusu Sadhvi
Sadhvi Deva Thakur
Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.
Kwenye video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katia jimbo la Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi akitumia bunduki aina ya revolver.
Baadhi ya walinzi wake nao wanaonekana wakifyatua risasi.
Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa Sadhvi, ambalo ni jina la kiindi linalomaanisha mwanamke aliye mtakatifu au anajiita kuwa mungu alingia sakafuni, ambapo alimuomba DJ kucheza wimbo aliotaka na akaanza kucheza densi.
Wakati huo ufyatuaji risasi ulikuwa ukiendelea.
Ripoti zinasema kuwa familia za bibi na bwana harusi zilimuomba awache maombi yao yaliambulia patupu.
Sadhvi ana wafuasi wachache ambao wengi wengi ni kutoka kijijini
akiwa na wafuasi wake
Ni wakati shangaziye bwana Harusi mwenye umri wa miaka 50 aliangauka baada ya kupigwa rasasi na wengine watatu kujeruhiwa vibaya, ndipo ufyatuaji huo ukasitishwa.
Wakati huo Sadhvi na walinz wake sita walitoweka. Polisi wamewafungulia kesi ya mauaji na wanajaribu kuwatafuta watu hao saba.
Source:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here