Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,
“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule”alisema Mashinji.
Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.
Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.
No comments:
Post a Comment