Kocha mpya
wa Yanga, George Lwandamina amesema ameanza kazi yake vizuri akiwa anategemea
ushirikiano mkubwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hans van der Pluijm.
Lwandamina
amesema, siku ya kwanza tu imemuonyesha mwanga kwamba mambo yatakwenda vizuri
lakini ni lazima wafanye kazi kwa juhudi.
“Tutafanya
kazi kwa juhudi na ushirikiano wa juu kabisa. Tumeanza vizuri na umeona morali ya
wachezaji iko juu,” alisema.
Yanga
ilianza mazoezi yake kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam na
Pluijm na Lwandamina wote walionekana wakiwa kazini pamoja.
No comments:
Post a Comment