FIFA imetangaza Wagombea Watatu wa mwisho kutoka Listi ya Wachezaji 23 wa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016.
Watatu hao ni Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid), Antoine Griezmann (France/Atletico Madrid) na Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona).
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea ni Melanie Behringer (Germany/FC Bayern Munich), Carli Lloyd (USA/Houston Dash) na Marta (Brazil/FC Rosengård).
Kwa upande wa Makocha, Wagombea wa mwisho pia wametajwa na kwa Wanaume ni Claudio Ranieri (Italy/Leicester City), Fernando Santos (Portugal/Timu ya Taifa ya Portugal) na Zinedine Zidane (France/Real Madrid)
Kwa apande wa Kinamama Wagombea ni Jill Ellis (USA/Timu ya Taifa ya USA), Silvia Neid (Germany/Timu ya Taifa ya Germany) na Pia Sundhage (Sweden/Timu ya Taifa ya Sweden).
KURA KUPATA WASHINDI:
-Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:
-Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama FIFA
-Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za Mashabiki
-Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka Mabara yote 6 Duniani.
Vilevile Wagombea Watatu wa Goli Bora la Mwaka wametangazwa kutoka 10 wa awali na hao ni Marlone (Brazil/Corinthians), Daniuska Rodriguez (Venezuela/Venezuela Timu ya Taifa ya Wanawake U-17) na Mohd Faiz Subri (Malaysia/Penang).
Washindi wa Tuzo hizo za Ubora watatangazwa rasmi Januari kwenye Hafla maalum ya FIFA.
No comments:
Post a Comment