Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema kuwa wanafunzi 526,653 kati ya 555,291 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwakani katika shule za sekondari za Serikali.
Kwa
mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni sawa na asilimia 94.85
ya wanafunzi wote waliofaulu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari tarehe 28 Novemba 2016 mjini Dodoma Waziri
Simbachawene ameeleza kuwa wanafunzi 28,638 wakiwemo wavulana 12,937 na
wasichana 15,701 hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi.
Aidha
Waziri Simbachawene aliitaja mikoa ambayo wanafunzi wake walifaulu
lakini hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na Dar Es
Salaam (18,820), Arusha (4,752), Songwe (1,465), Kigoma (1,208), Manyara
(1,141), Lindi (608), Mbeya (406) na Katavi (238).
Kuhusu
wanafunzi waliochaguliwa Waziri Simbachawene amesema kuwa, wasichana ni
268,052 sawa na asilimia 94.5 na wavulana ni 258,601 sawa na asilimila
95.2.
Aidha,
Waziri wa Nchi amesema kuwa wanafunzi wote wenye ulemavu waliofaulu
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2017.
Kwa
mujibu wa Waziri Simbachawene mchanganuo wa wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali umegawanyika katika
makundi manne ambapo kundi la kwanza limehusisha wanafunzi 900 wakiwemo
Wavulana 480 na Wasichana 420 ambao wamepelekwa katika shule za Bweni
kwa wenye ufaulu mzuri zaidi.
Ameongeza
kuwa kundi la pili limehusisha wanafunzi 1005 ikiwa ni Wavulana 915 na
Wasichana 90 ambao wamepelekwa katika shule za Bweni mahsusi kusomea
Ufundi.
Pia
amesema kuwa kundi la tatu limewahusisha Wanafunzi 780 wakijumuishwa
Wavulana 430 na Wasichana 350 ambao wamechaguliwa kujiunga na Shule za
Bweni Kawaida na kundi la nne limewahusisha wanafunzi 723 wakiwemo
wavulana 405 na wasichana 318 wa shule za bweni kwa ajili ya wanafunzi
walio na Ulemavu.
Kulingana
na takwimu hizo, Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya wanafunzi
3,407 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni kidato cha kwanza ambapo
wavulana ni 2,230 sawa na asilimia 65.4 na wasichana 1,178 sawa na
asilimia 34.6, pia watahiniwa wapatao 6,260 sawa na asilimia 0.78 ya
waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
Aidha
Waziri Simbachawene amesema kuwa wanafunzi 523,245 wakiwemo wavulana
256,371 na wasichana 266,874 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule za kutwa.
Wakati
huo huo Mhe. Simbachawene amesema hatasita kuzichukulia hatua, shule
zilizohusika na udanganyifu wa mitihani kwani wanarudisha nyuma
maendeleo ya taaluma nchini yanayofanywa na Serikali.
“Serikali
imeanza kuwachukulia hatua kwa mujibu wa taratibu wale wote waliohusika
na udanganyifu huu� hatua hizo ni pamoja na kuwavua madaraka waliokuwa
Waratibu Elimu Kata na Walimu Wakuu, kuwashtaki mahakamani na kupeleka
mashauri yao Tume ya utumishi ya Walimu (TSC),” amesema Mheshimiwa
Waziri.
Pia
ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kubainisha sababu za wanafunzi
walioingia darasa la kwanza kutomaliza masomo yao kama ilivyotarajiwa.
“Naagiza
Wakuu wa Mikoa kubainisha sababu za wanafunzi hao kutomaliza na hatua
stahiki za kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote
wanaoandikishwa darasa la kwanza wanamaliza mzunguko wa masomo kwa
mujibu wa Sera ya Elimu,” amesisitiza Mhe. Simbachawene na kutaka Wakuu
wa mikoa kuchukua hatua stahiki zilizoelekezwa.
No comments:
Post a Comment