Korea Kaskazini: Tunauwezo wa kuifumua Marekani yote - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, July 29

Korea Kaskazini: Tunauwezo wa kuifumua Marekani yote


Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa jaribio hilo lilibaini kwamba marekani yote ipo katik radara ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa, vyombo vya habari vimeripoti.

Jaribio la kombora hilo linajiri wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu la Korea Kaskazini.

Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini .

China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pandfe husika zilizo na waiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi.

Ikithibtisha kurushwa kwa kombora hilo, Korea Ksakzini ilisema kuwa kombora hilo la masafa marefu liliruika kwa dakika 47 na kufika urefu wa kilomita 3,724

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here