Mchezaji wa tenisi avunjika goti uwanjani - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, July 7

Mchezaji wa tenisi avunjika goti uwanjani


Marekani. Mcheza tenisi wa Marekani, Bethanie Mattek-Sands amevunjika goti wakati akiwa uwanjani wakati wa mchezo kwenye mashindano ya Wembledon.

Mchezaji huyo ambaye ni mshindi wa mara tano wa mashindano ya tenisi ya wanawake yanayojulikana Grand Slam, aliumia katika raundi ya pili ya mchezo na kuanguka ghafla, huku akiangua kilio uwanjani kutaka msaada wa haraka.

Mcheza tenisi maarufu Luice Safarova alikuwa ni miongoni mwa watazamaji waliokuwapouwanjani hapo na alimwaga chozi wakati akishuhudia mchaji huyo akiugulia maumivu uwanjani huku akipatiwa huduama ya kwanza.

Bathanie mwenye miaka 32 alianguka wakati akiukimbilia mpira ili kuurudisha kwa mpinzani. Tukio hilo lililozua taharuki kwa watazamani uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here