IDARA ya Afya, wilayani Igunga imepiga marufuku wananchi kuingia na mifuko ya rambo hospitali ili kuepusha vyoo kuziba.
Ofisa afya wilaya, John Masesa, alisema wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona mifuko hiyo kutumiwa na baadhi ya watu wanapojisaidia kwenye vyoo vya hospitali na kusababisha kuziba.
Alisema pamoja na uongozi wa hospitali kuweka maji ya kutosha kwenye vyoo, baadhi yao wananchi hawayatumii na badala yake kutumia mifuko hiyo.
Alisema mtu yoyote atayebainika kuingia na mifuko hiyo atatozwa faini ya Sh. 50,000 na kuwataka wananchi kuzingatia sheria za nchi.
Mzabuni anayefanya usafi katika hospitali hiyo, Amina Nsalale, alisema kupigwa marufuku kwa mifuko hiyo, kutasaidia kupunguza uchafu.
Ofisa usafi na mazingira, Fredrick Mnahela, alisema suala la usafi sio la serikali pekee.
Aidha Mnahela alisema halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/2018, imejipanga kujenga vizimba 13 vya kutunza taka ikiwa pamoja na kutafuta mzabuni atakayekusanya uchafu kwa ngazi ya kaya na kuzipeleka katika vizimba hivyo.
No comments:
Post a Comment