Kwenye Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM leo July 6, 2017 mtangazaji Geah Habibu ametuletea inayomuhusu mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kujiua baada ya mkewe kuchukua mikopo mingi na kushindwa kulipa jambo lililosababisha kuandamwa sana akidaiwa.
Tukio hilo limetokea Shinyanga ambapo inadaiwa mwanaume huyo alikuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara kwa ajili ya shughuli zake na alikuwa anatuma hela kila alipohitaji kufanya hivyo lakini mkewe alizitumia vibaya hata kumpelekea kukopa na kulimbikiza madeni jambo lililopelekea auze vitu vya ndani.
Baada ya mumewe kurudi nyumbani alikuta madeni na ndani hakuna vitu hivyo ukazuka ugomvi ambapo alimuuliza mkewe alikuwa anazifanyia nini hela mpaka akafikia hatua ya kukopa na kuuza vitu vya ndani. Kutokana na kukosa majibu ugomvi huo uliendelea kila siku hata mwanamke akaamua kuondoka nyumbani ambapo baada ya siku mbili mwanaume aliamua kujinyonga.
No comments:
Post a Comment