Chelsea yamwambia Costa arejee London haraka kuanza mazoezi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 15

Chelsea yamwambia Costa arejee London haraka kuanza mazoezi


KLABU ya Chelsea imemtaka mshambuliaji wake, Diego Costa kurejea London haraka iwezekanavyo kuanza mazoezi ili kuwa fiti kuwa fiti kwa ajili ya mechi ili arejeshwe kikosi cha kwanza.

Wazi hizi ni dalili nzuri kwamba tofauti za Costa na kocha Antonio Conte zinaelekea kumalizika.
Uhusiano wa wawili uliingia doa baada ya Conte kumuandikia ujumbe kwenye simu ya mkononi Costa Juni mwaka huu kumuambia mfungaji huyo wa mabao 20 msimu uliopita kwamba hayuko katika mipango yake ya msimu mpya.

Conte alisema uamuzi huo ulichukuliwa Januari wakati Costa alipokuwa anataka kuhamia China na akaondolewa kikosini baada ya kukorofishana na kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, Julio Tous.

Tangu hapo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akaamua bora arejee Atletico Madrid, lakini klabu haijawahi kufikiria kumruhusu kuondoka.

Mazungumzo yameibuliwa tena na wanasheria wa Costa wanataka aruhusiwe kama mchezaji huru, kwa sababu mkataba ulikwishavunjwa na ujumbe wa Conte kenye simu. Kwa Chelsea, ambayo inamthaminisha mshambuliaji huyo wa kimataifa Hispania kwa dau la Pauni Milioni 60, kwa sasa ipo hatarini kumpoteza bure mchezaji huyo.

Costa aliruhusiwa kuripoti wiki moja baadaye kwa maandalizi ya msimu mpya, huku klabu ikijadiliana na Atletico kabla yaa baadaye kuenguliwa kwenye ziara za China na Singapore.

Costa kwa sasa yuko nyumbani kwa, Lagarto nchini Brazil na katika mahojiano maalum na Waandishi wa Habari akasema Chelsea ilimfanyia kama mhalifu na ndiyo maana ameamua kubaki peke yake Amerika Kusini kuliko kwenda kufanya mazoezi na wachezaji wa akiba mjini Surrey bila kuwa na matarajio ya kucheza.

"Hiki kinaonekana ni kitu kibaya sana na maisha mabaya,"amesema Costa. "Hawaheshimu ambayo nimeifanyia klabuI,". ameongeza.

Pamoja na hayo, Chelsea haiko tayari kumruhusu Costa kuondoka akiwa amebakiza mkataba wa miaka miwili anaolipwa Pauni 180,000 kwa wiki.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here