Wimbo umeimbwa na Diamond, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Maromboso, Lavalava na Queen Darleen, muimbaji Matonya leo kupitia ukurasa wake wa instagram kaandika ya moyoni kutokana na wasanii hao kutumia jina la wimbo wake pasipo kushirikishwa.
“Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini?”
“Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/ kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila woga🙆🙆🙆🙆 lakini haki itafata mkondo wake”
No comments:
Post a Comment