Mensen Selekta na DJ Tito wamshambulia Man Fongo - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, January 25

Mensen Selekta na DJ Tito wamshambulia Man Fongo



Msanii na mtayarishaji muziki kutoka studio ya Defatality Mensen Selekta pamoja na DJ Tito wamemshambulia kwa maneno muimbaji wa singeli Man Fongo kutokana na tabia yake ya kutafuta kiki kwa kutumia majina yao kila anapotaka kutoa kazi zake mpya.

Mensen na DJ Tito wameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya msanii huyo kusema 'biti' anayolalamikiwa kuwa ameiba kwamba amepewa na DJ Tito ambae yupo chini ya Mensen.

"Mimi naomba tu, nimekanye Man Fongo maana naona muziki wake hawezi kuufanya bila ya Mensen kwa sababu haiwezekani kila anapotaka kuachia ngoma au 'video' amzungumzie Mensen ameenda amerudi kwa nini hawezi kuwazungumzia watu wengine ?. Kwa hiyo inaonesha kabisha Man Fongo bila ya Mensen hamna kitu, suala la kutoa 'instrument' ninavyojua mimi 'biti' sikutoa mimi bali alitengeneza kijana wangu", alisema Mensen.

Aidha, Mensen Selekta aliendelea kufafanua baadhi ya mambo na kusema siyo kweli kama anavyodai Man Fongo kuwa mdundo huo unaolalamikiwa amemuibia Sholo Mwamba kuwa umetolewa na DJ Tito.

"Cha kwanza akanushe kauli yake, DJ Tito hajagawa 'biti' kwa sababu yeye siyo 'producer' halafu ninavyojua mimi hawana mahusiano ya karibu ya kihivyo na Man Fongo", alisisitiza Mensen Selekta.

Kwa upande wake DJ Tito alisema alifuatwa na Man Fongo ili aweze kutengeneza 'kiki' kupitia mdundo huo kwa kumtaka aseme yeye ndio aliyempatia ili Sholo Mwamba akasirike.

"Mimi siwezi kupenda kumwambia kitu kizuri Man Fongo, sema namuelekeza kimazingira tu lakini yeye anayumba halafu kigege 360 kipo kwa ajili ya kazi na kupambana ili mambo yaende, muziki haufanywi hivyo anakiuka mazingira ya kimuziki", alisema DJ Tito.

DJ Tito aliendelea kwa kusema "Man Fongo yeye afanye kazi nzuri tu mbona watanzania watampokea vizuri, halafu hichi kigege 360 ndicho kilichomlea ila yeye ameleta dharau kwa Mensen na kwangu mimi ambaye niliyemtoa Tandale kwa hiyo Man Fongo ana laana na laana siyo lazima upewe na Baba au Mama hata masela kama sisi tunakuachia laana na hausongi mbele".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here