MWENYEKITI wa kampuni ya
Kutengeneza matairi ya Pirelli, Marco Tronchetti Provera ambao ndio wadhamini
wakubwa wa Inter Milan amesema bado ana matumaini ataweza kutimiza ndoto za
kumleta Lionel Messi katika klabu hiyo kutoka Barcelona.
Nyota huyo wa kimataifa wa
Argentina kwa mara nyingine mustakabli wake umeleta mjadala mkubwa katika wiki
za karibuni huku kukiwa na tetesi kuwa mazungumzo hayaendi kama yalivyotarajiwa
Camp Nou.
Taarifa zinadai kuwa mkurugenzi
wa michezo wa Paris Saint-Germain-PSG Patrick Kluivert ameshazungumza na baba
yake ya Messi kujadili uwezekano wa nyota huyo kwenda kwa mabingwa hao wa Ligue
1.
Pamoja na hayo, Messi mwenyewe
mara zote amekuwa akisisitiza kuwa anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya
utotoni ya Newell’s Old Boys ya Argentina wakati muda wake Barcelona
utakapomalizika.
Provera amesema lengo lake ni kumshawishi nyota huyo mwenye
umri wa miaka 29 kufikiria kuichezea Inter.
No comments:
Post a Comment