Na Mustafa Ismail
Watanzania
na wadau wakuu wa sekta binafsi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano
wa wadau wa uendelezaji wa viwanda vya usindikaji utakao fanyika jumamosi ya
terehe 3 desemba mwaka huu katika ukumbi wa mwalimu nyerere convention centre
jijini Dare es salaam
Akiongea na
waandishi wa habari Jijini daresalaam mwenyekiti wa chama cha {Tanzania Food
Processors association [TAFOPA]} Suzy Laiser mewataka wadau kujitokeza katika
mkutano huo utakao hudhuriwa na washiriki takariban mia moja wakiwemo mawaziri
wa wizara mbalimbali, wawakilishi wa mikoa, wakurugunzi wa halamashauri;
wakurugenzi wa mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo sekta binafsi na
mashirika yasiyo ya kiserikali.
Laiser
amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzindua uanzishwaji wa uendelezaji wa
maeneo ya viwanda vya usindikaji[Food Processing Industrial Parks] kuhamasisha
na kutafuta washirika kutoka katika mshirika ya kimataifa serikali na sekta
binafsi.
Aidha Laiser
aliongeza kuwa mkutano huo utakuwa fursa pekee ya kushughulikia changamoto
zinazowakabili wasindikaji wa vyakula nchini “changamoto kubwa ya wasindikaji
ni maeneo safi na salama ya kusndikia kwani wengi wanasindikia majumbani hivyo
basi wanakabiliwa na changamoto za kukidhi viwango vya kitaifavta ubora na
usalama wa chakula”
Naye
mtaalamu na mshauri wa chama hicho Gloria Kavishe amesema kuwa chama kina
malengo ya kuhakikisha bidhaa zinazotolewa na chama hicho zinasambazwa kote
nchini na nje ya nchi “tumalengo yakusambaza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi
kwani tunatarajia kupata mitambo ya kutosheleza na yenye hadhi ya juu”
Aidha
Kavishe aliongeza kuwa mkutano huo unaunga mkono juhudi za Mama Samia Suluhu
Hassan za kuendeleza “cottage industry” kama mkakati wa kuwawezesha wanawake
kiuchumi.
Mkutano huo
utaongozwa na Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia
Suluhu Hassan aliyeteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuwa mwakilishi wa mashariki na kusini katika
mkakati wa kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Chama hicho
chenye wanachama zaidi ya 600 kimetoa mafunzo ya usindikaji kwa takriban watu
7000 na kina lenga kutoa mafunzo zaidi.
No comments:
Post a Comment