Baada
ya kusaini miaka miwili kuichexea Yanga, kiungo mkabaji wa timu hiyo,
Justine Zulu jana Ijumaa alipewa jezi namba 14 na kuanza mazoezi na
wenzake. Jezi namba 14 inatajwa kuwa na mikosi katika kikosi hicho.
Jezi
hiyo, ina sifa moja pekee ambayo kila mchezaji mpya atakayeivaa huwa
hadumu kwenye timu muda mrefu na badala yake kujikuta anatemwa au kuanza
na wakati mgumu.
Kati
ya wachezaji waliowahi kuivaa jezi hiyo na kudumu kwa kipindi kifupi ni
kiungo mshambuliaji raia wa Niger, Issofou Boubacar aliyedumu na timu
hiyo kwa miezi sita pekee kwenye msimu wa 2015/2016, pia beki wa kati
Rajab Zahiri aliyeitumikia kwa msimu mmoja na nusu.
Taarifa
zinaeleza kwamba, Zulu anayefahamika pia kama mkata umeme kutokana na
sifa yake ya uhodari wa kukaba na kuanzisha mashambulizi, yeye mwenyewe
ndiye aliyeomba apatiwe jezi hiyo.“Zulu
amepewa jezi namba 14 mara tu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
ya kuichezea Yanga, ataanza kuonekana nayo kwenye mzunguko wa pili wa
ligi kuu.
“Jezi
hiyo, yeye mwenyewe ndiye aliyeiomba kabla ya viongozi kumpa na kuanza
kuivaa kwenye mazoezi ya leo (jana) jioni kwenye viwanja vya Gymkhana,”
alisema mtoa taarifa huyo.
Meneja
wa timu hiyo, Hafidh Saleh kuzungumzia hilo, alisema: “Hizo taarifa ni
za kweli, Zulu nimempa jezi namba 14 aliyoiomba yeye mwenyewe,” alisema
Saleh.
Zulu jana jioni alivaa jezi hiyo katika mazoezi ya timu yake kwenye Viwanja vya Gymkhana chini ya Kocha George Lwandamina.
Katika
mazoezi hayo, Zulu alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mpira na
kukaba huku akipiga pasi nyingi za visigino kiasi cha kushangiliwa na
mashabiki wachache waliokuwepo nje ya uzio wa uwanja huo.
No comments:
Post a Comment