Kwa kawaida ilivyo kama ukimwaga mboga basi wenzio wanamwaga ugali na ndivyo ilivyo katika kikosi cha wekundu wa msimbazi,Simba SC baada yakuona kiungo wao Jonas Mkude haeleweki katika kusaini upya mkataba wake na klabu hiyo.
Simba inaona Mkude anadengua kusaini mkataba mpya wao watamsajili kiungo mwenye uwezo zaidi yake.
Achana
na hiyo, Simba pia imepanga kumpiga benchi Mkude katika michezo yao
inayokuja ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kwani haijapendezwa na
kitendo cha nahodha huyo kusema yupo tayari kusaini hata Yanga kama
atazinguliwa na timu yake hiyo.
Tayari
Mkude amevuka mtego wa kwanza aliowekewa na Simba kwamba kama
asingetokea mazoezini angekatwa mshahara wake lakini kiungo huyo ameenda
mara moja katika mazoezi hayo ambapo jana ilikuwa siku ya nne ya
mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es
Salaam.
Mmoja
wa mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba, amesema: “Tunataka kumsajili
kiungo mkabaji mwingine katika usajili huu, haya mambo ya Mkude
hayajatupendeza.”
“Inaonekana
Mkude anatudengulia kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili kutoka
ule wa sasa ambao unaisha Januari mwakani, awali tulipanga kuongeza beki
wa kati, beki wa kulia na kipa pekee.
“Lakini
baada ya Mkude kutudengulia kusaini mkataba, tumeona ni bora
tukamsajili kiungo mwingine mwenye uwezo kama wake, hatutaki tuwe na
mchezaji mmoja tegemeo kwenye timu,” alisema bosi huyo.
Zacharia
Hans Poppe ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
akizungumzia hatua hiyo, alisema: “Tunaendelea kufanyia kazi ripoti
tuliyokabidhiwa na kocha wetu, hayo mengine tutaangalia baadaye.”
Awali,
Mkude amesema kuwa, hajawahi kuzungumza na viongozi wake kuhusu mkataba
mpya na anashangaa kuhusu kuelezwa kwamba hapatikani hewani.
Kuhusu
kuwazimia simu viongozi wa Simba, Mkude alisema: “Ndiyo nilizima simu
kwani wao walisema mimi nimeshasaini mkataba mpya wakati si kweli, hivyo
nikawa napata usumbufu kwa ndugu wengine wakitaka kujua sababu za mimi
kufanya hivyo bila kuwashirikisha na wengine waliniomba fedha wakati si
kweli. Haikuwa haki.”
Usajili wa dirisha dogo unaoendelea sasa, ulianza Novemba 15, mwaka huu na unaisha Desemba 15.
source:SalehJ
No comments:
Post a Comment