Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane amesaini mkataba mpya na klabu ya Tottenham ambayo itamfanya kusalia kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2022.
Mkataba huo, umeripoti kuwa mchezaji huyo atapokea kitita cha zaidi ya pauni elfu 100 kwa wiki. Mkataba huo mpya utachukua nafasi ya mkataba aliokuwa ameutia sahini mwezi Februari mwaka wa 2015.
''Kila mmoja anajua kile ninachokihisi kwa klabu hii, amesema Kane, 23, ambaye amefunga magoli matano kwa mechi 17 alizoshiriki katika timu ya taifa ya England.
''Kutia sahini mkataba mwengine,una hisia maalum.Tuna kikosi kikali cha wachezaji wachanga na klabu yenyewe inaelekea katika njia bora.''
Kane amefunga mabao 6 katika mechi 10 alizoshiriki na klabu hiyo ya Spurs msimu huu, licha ya kukosa kushiriki mechi 10 kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.
Mshambuliaji huyo amefunga mara 21 katika msimu wa 2014-15 na kushinda viatu vya dhahabu kwa kufunga magoli 25 msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment